78. KlKATI -IST-.
Kiambishi hicho cha ndani hutumika kuonyesha afanyaye kazi
fulani kwa mshahara. Tazama mifano hii:
mchungaji
|
paŝtist-o, -ino
|
kuchunga
|
paŝti
|
mwimbaji
|
kantist-o, -ino
|
kuimba
|
kanti
|
mchoraji
|
pentrist(in)o
|
kuchora
|
pentri
|
mpagazi
|
portist(in)o
|
kupagaa
|
porti
|
mlezi
|
vartist(in)o
|
kulea
|
varti
|
mwizi
|
ŝtelist(in)o
|
kuiba
|
ŝteli
|
mfanya kazi
|
laborist(in)o
|
kufanya kazi
|
labori
|
kiongozi
|
gvidist(in)o
|
kuongoza
|
gvidi
|
hakimu,
jaji
|
juĝist(in)o
|
kuhukumu
|
juĝi
|
79. ZOEZI
Andika majina ya wafanyakazi wa kiume na wa kike yanayoweza
kutokana na maneno haya yafuatayo: boto (buti), dento (jino), baki
(kuoka).
Tafsiri:
ĉapelisto, floristo, ĝardenisto, vendisto,
lignisto (lign- = kipande cha mti, ukuni).
Rudia maneno ya hapa juu ukitumia kikati -in-,
halafu tafsiri maneno haya mapya.
80. KlKATI –IL-.
Kikati hiki huonyesha chombo ambacho hufanywa kazi kwa njia
yake: zana, ala:
kifunguo
|
ŝlosilo
|
kufungua
|
malŝlosi
|
mtego
|
enkaptilo
|
kutega
|
enkapti
|
ponyo
|
kuracilo
|
kuponya
|
kuraci
|
shoka
|
hakilo
|
kutema
|
haki
|
sindano ya kushonea
|
kudrilo
|
kushona
|
kudri
|
rula
|
liniilo
|
mstari
|
linio
|
mchezo
|
ludilo (kititia)
|
kucheza
|
ludi
|
kisu
|
tranĉilo
|
kukata
|
tranĉi
|
81. PER = kwa, kwa njia ya, na.
Aliua nyoka kwa bunduki = Li mortigis serpenton per
pafilo.
82. ZOEZI
Tafsiri:
Ni hakas per hakilo. Kial vi kombas viajn harojn per
forko, kaj ne per kombilo? Tio estas la viŝilo, per kiu mi viŝas la
tabulon.
83. ZOEZI
Ukitumia maneno haya hapa chini pamoja na kikati cha zana -il-
tafsiri sentensi zifuatazo maneno yenyewe: tondi (kunyoa), fosi (kuchimba),
presi (kuchapa), segi (kupasulia);
Wote hunyoa kwa
mkasi. Wote huchimba kwa sepetu. Wote huchapisha kwa mtambo wa kupigia
chapa. Wote hupasulia kwa msumeno.
Fuata mfano huu:
Wote hunyoa kwa mkasi = Ĉiuj tondas per
tondilo.
84. KIKATI -AR-
Kikati hiki huonyesha jumuiko au mkusanyiko wa viumbe vyenye
aina moja tu:
arbo
|
mti
|
arbaro
|
msitu, mwitu
|
kampo
|
shamba
|
kamparo
|
shamba
|
libro
|
kitabu
|
libraro
|
maktaba, jumuiko la vitabu
|
mapo
|
ramani
|
maparo
|
atlasi
|
ŝtupo
|
kipago, kidaraja
|
ŝtuparo
|
ngazi
|
vagono
|
behewa
|
vagonaro
|
gari la moshi
|
vorto
|
neno
|
vortaro
|
kamusi
|
85. ZOEZI
Tafsiri ukitumia kikati -ar-:
jamii ya rafiki, kundi la ng'ombe, jamii ya vyumba, kundi la
ndugu, diwani la nyimbo, kundi la vijana, kundi la kondoo, jamii ya meli.
86. VIELEZI VYA WAKATI
Mpaka sasa umeshajifunza maneno: baldaŭ, nun,
hieraŭ, hodiaŭ, morgaŭ. Maneno haya huonyesha kitendo wakati
kilipotendeka. Tunaita maneno haya "vielezi vya wakati".
Jifunze mengine:
ĉiam = daima, milele, bila ya kukoma
neniam = abandani, kamwe, hata mara
moja
jam = zamani.
ANGALIA
kwamba:
- kielezi
neniam havitumiki kama kitenzi cha Kiesperanto ni katika
hali ya kutotenda
- wazo
la "hata kidogo" linatolewa kutoka katika Kiesperanto kwa neno neniom
siyo kwa neno neniam.
Chungua matumizi
ya vielezi vya wakati katika sentensi zifuatazo:
Li jam venis.
|
Amekwisha fika.
|
Mi jam pagis
|
Nimelipa zamani.
|
Tiu homo neniam kontentiĝas.
|
Mtu huyu haridhiki abadani.
|
Mi neniam venos.
|
Sitakuja abadani.
|
87. ZOEZI
Tafsiri:
Ĉu vi baldaŭ venos? Jes, mi venos hodiaŭ.
Ĉu la teo estas preta nun? Mi jam skribis du leterojn. Kiu venos morgaŭ? Kial la ĝardenisto
ne venis hieraŭ? Hodiaŭ mi aĉetos segilon. Mi jam havas tranĉilon. Mi neniam uzis hakilon. Ne nun, sed
baldaŭ. Mi ĉiam kantas kiam mi estas feliĉa.
88. VIELEZI
Kwa jumla vielezi ni maneno yanayoeleza vile vitendo
vilivyotendeka, yaani yaeleza kitendo jinsi kilivyotendeka, mahali kilipotendeka,
wakati kilipotendeka, n.k.
Tukisema: "amekuja polepole", "unasoma
vizuri", "ameingia hapa", "njoo kesho",
n.k. huwa tumetumia vielezi; yaani:
-
kielezi cha mahali (huonyesha kitendo mahali kilipotendeka): hapa.
-
kielezi cha wakati (huonyesha kitendo wakati kilipotendeka): kesho.
-
vielezi vya namna (huonyesha kitendo jinsi kilivyotendeka): polepole,
vizuri.
Hapa chini vipo vielezi kadhaa vya namna:
bele
|
vizuri
|
lerte
|
kwa ustadi
|
bone
|
vyema
|
malbone
|
vibaya, kwa kosa
|
hele
|
kwa uangavu
|
simple
|
tu, peke yake,
rahisi
|
89. KIAMBISHI –E.
Uliposoma vielezi vilivyopita uligundua kwamba maneno haya
yote (yaani ya kifungu cha 88) huwa yametumia kiambishi kile kile: -e.
Basi, kwa Kiesperanto kila neno likitumia kiambishi tamati -e linaweza kufanya kazi ya kielezi. Pia kila kielezi cha namna lazima kiwe na
kiambishi hicho cha -e. Kwa mfano:
rapida
|
(mzizi: rapid)
|
-epesi, -a upesi
|
rapide
|
upesi
|
saĝa
|
(mzizi: saĝ)
|
-a busara
|
saĝe
|
kwa busara
|
Vielezi
vyenye kiambishi -e ulivyovisoma mpaka sasa ni: eble,
kompreneble, efektive.
90. ZOEZI
Tafsiri vielezi vifuatavyo:
kwa utamu, kwa wazi (au: kwa dhahiri), kwa kelele (au: kwa
sauti kubwa), kwa polepole (au: kinyerenyere), kwa kweli (au: kwa moyo,
kiaminifu),
kwa kutumia
maneno ya orodha ya hapa chini:
dolĉa -tamu
klara wazi, dhahiri
laŭta -a kelele, -enye sauti kubwa
malrapida polepole
sincera aminifu