46. RANGI, koloroj
blanka |
-eupe |
lazura |
ya samawi |
blua |
-a buluu |
nigra |
-eusi |
bruna |
ya kahawa |
oranĝa |
ya manjano mabivu |
flava |
ya manjano |
ruĝa |
-ekundu |
griza |
ya kijivu, ya jivu |
verda |
ya kijani, ya majani |
Tumia maneno haya juu ukitunga sentensi kumi kama mfano ufuatao:
Kia estas la koloro de banano? Banano estas flava.
47. NAMBARI, numeroj
1 |
2 |
3 |
4 |
5 |
6 |
7 |
8 |
9 |
10 |
unu |
du |
tri |
kvar |
kvin |
ses |
sep |
ok |
naŭ |
dek |
11 dek unu |
12 dek du |
13 dek tri |
... |
19 dek naŭ |
|
20 dudek |
30 tridek |
... |
90 naŭdek |
21 dudek unu |
32 tridek du |
43 kvardek tri |
... |
99 naŭdek naŭ |
100 cent
101 cent unu
111 cent dek unu 122 cent dudek du 133 cent tridek tri ... 999 naŭcent naŭdek naŭ
1000 mil
1001 mil unu ... 1011 mil dek unu ... 1111 mil cent dek unu ...
48. UPANGAJI WA KIVUMISHI
Angalia kwamba upangaji wa kivumishi cha sifa ya kuhesabia ni tofauti kabisa na ule wa Kiswahili: kivumishi hicho hutajwa kabla
ya jina lenyewe:
|
Du birdoj en unu kaĝo. |
Ndege wawili ndani ya kitundu kimoja. |
Ukitaka kueleza jina moja kwa kutumia vivumishi viwili au zaidi, upangaji wa vivumishi vya mchanganyiko huo ni karibu kinyume
cha upangaji wa Kiswahili. Soma tena kifungu cha 17.
49. ZOEZI
Tafsiri:
La tri knabinoj ludis en la gardeno (bustani). Sur la seĝo (kiti) estis
kvar libroj kaj du plumoj. Ses aŭ sep glasoj estas sur la tablo. En la
strato (njia) estas ducent domoj (nyumba).
La domo staras inter (katikati ya) du arboj.
50. ZOEZI
Kamilisha sentensi zifuatazo kwa kutumia maneno na nambari za mwishoni. Fanya kama mfano:
Sur la tablo estas .......................................................... (5/libroj).
MFANO: Sur la tablo estas kvin libroj.
En la ĉambro estas ....................................................... (3/virinoj).
En la klas-ĉambro sidas .................................................
(16/infanoj).
Sur la breto (rafu) estas
.................................................. (7/vazoj).
Sasa tafsiri sentensi zote ulizozikamilisha na sentensi zifuatazo:
En unu jaro (mwaka) estas dek
du monatoj (miezi). Kiu numero
venas post (hufuata) ses? Kiu numero venas antaŭ (hutangulia) dek
tri? Kiu numero venas inter sep kaj naŭ?
2 + 3 =5 |
Du kaj tri estas kvin. AU: Du plus tri estas kvin. |
5 - 2 = 3 |
Kvin minus du estas tri. |
6 : 2 = 3 |
Ses one je du estas tri. AU: Duone ses estas tri. AU: Ses duone estas tri. |
4 x 7= 28 |
Kvaroble je sep estas dudekok. AU: Sepoble kvar estas dudek ok.AU: Kvar sepoble estas dudek ok. |
51. VIULIZI:
Kiom? |
-ngapi? (bila jina) |
Kiom da ...oj? |
-ngapi? Kiasi gani cha ... ? -ngapi -a ...? (kinafuatwa na jina) |
Chungua mifano ifuatayo:
Kiom estas 2 + 2? Mbili kuzidisha mbili ndio ngapi?
Kiom da mono pags Daudi? Daudi alilipa kiasi gani cha fedha?
Kiom da mangoj li kolektis sub tiu arbo? Aliokota embe ngapi chini ya
mti ule?
Jibu kwa Kiesperanto:
Kiom estas 5 + 6? Kiom
estas 4 + 9? Kiom estas 16 - 8? Kiom
estas 4 x 9? Kiom estas 15: 5? sasa jibu ukitumia
sentensi za kifungu cha 50.
Kiom da libroj estas sur la
tablo? Kiom da virinoj estas en la ĉambro? Kiom da vazoj estas sur la
breto? Kiom da infanoj sidas
en la klasÂĉambro? Kiom da monatoj estas en unu jaro?
52. MTENDAJI NA MTENDEWA
Katika
sentensi "anaona" ile "a" ya mwanzoni
yaonyesha anayefanya tendo. Tumeshaona kwamba kwa Kiesperanto badala ya ile
alama ya nafsi ya mtendaji (k.m. ile "a" katika "anaona")
hutumika kiwakiÂlishi au jina lenyewe la mtendaji:
ile "Ŝi" ni kiwakilishi cha mtendaji.
Zaidi
ya hayo, mara nyingi neno la tendo, yaani kitenzi, katika Kiswahili huwa na
sehemu nyingine inayoonyesha mtu au kitu kinachotendewa kitendo chenyewe,
yaani alama ya nafsi ya mtendewa. Alama hii hutiwa katikati ya kitenzi chenyewe
na huitika kikati cha mtendewa. Ile "wa" katika "anawaona"
yaonyesha mtendewa huyo. Kwa Kiesperanto hutumika kiambishi tamati -n
mwishoni pa kiwakilishi au mwishoni pa jina lenyewe la mtendewa:
Angalia
kwamba mara nyingi, hasa kwa jinsi ya kufanyia, matumizi ya alama za mtendewa
yanatofautiana sana katika lugha hizo mbili (rudia pia kifungu cha 34):
Mi amas. |
Ninapenda. |
Mi amas vin. |
Ninakupenda. |
Mi skribas. |
Ninaandika. |
Mi skribas al vi. |
Ninakuandikia. |
Mi skribas leteron al vi. |
Ninakuandikia barua. |
Angalia
kwamba alama ya mtendewa hutumika pia mwishoni pa viulizi hivi: kia,
kie, kio, kiu.
Matumizi
halisi ya alama hiyo utajifunza utakaposoma sarufi nyingine, kwa sasa chungua
mifano ifuatayo:
Ŝi vidas. |
Anaona. |
Kiu vidas? Ŝi. |
Nani anaona? Yeye. |
Ŝi vidas arbon. |
Anaona mti. |
Kion ŝi vidas? Arbon. |
Anaona nini? Mti. |
Li vokas. |
Anaita. |
Kiu vokas?Li. |
|
Li vokas ŝin. |
Anamwita. |
Kiun li vokas? Ŝin. |
|
Mi dankas vin. |
Ninakushukuru. |
Li vidas ilin. |
Anawaona. |
Mi donas al vi... |
Ninakupa ... |
53. ZOEZI
Tafsiri.
Mi amas vin. La infano amas
ĉokoladon (chakleti). La patrino
legas libron. La patro skribas leteron. La infano ludas futbalon (mchezo wa mpira). La instruisto amas la lernantojn.
54. VITENZI AKALI
aĉeti |
kununua |
lerni |
kujifunza |
trinki |
kunywa |
aŭdi |
kusikia |
manĝi |
kula |
tuŝi |
kugusa |
havi |
kuwa na |
puni |
kuadhibu |
vendi |
kuuza |
helpi |
kusaidia |
rompi |
kuvunja |
viŝi |
kufuta |
55. ZOEZI
Tafsiri:
Ĉu vi amas min? Kion vi havas en la mano? Ĉu vi vendis dek bananojn aŭ dudek? Kiu manĝis oranĝojn
en la lernejo (shule)? Ĉu vi aŭdas tion? Ĉu vi helpis la knabinojn? Kiu rompis la
seĝon? Kion vi trinkas? Kie estas
la libro, kiun (ambacho) vi aĉetis?