36. MASWALI
Umejifunza
viulizi vinne ambavyo hutumika kuulizia swali:
KIA? (-a
aina gani?) hutumika kwa kuuliza kuhusu sifa
KIO? (nini?) hutumika kwa
kuuliza kuhusu kitu au kazi ya watu.
KIE? (-pi?) hutumika kwa kuuliza kuhusu mahali (wapi?
mahali gani?)
KIU? hutumika kwa kuuliza kuhusu
mtu (nani?) au kama -pi katika sentensi kama hiyo:
Kalamu ipi ni yako?
KIU plumo estas (la) via?
Neno
jingine Ĉu pia hutumika kuulizia swali, bali neno hutumika
kama jibu itakuwa "Ndiyo!" (Jes !) au "Hapana!" (Ne!), pia kiulizi Ĉu huwa hakitumiwi mwanzoni mwa
maswali yenye viulizi hivi juu (vyenye kianzio K-). (Mara
kwa mara kwa Kiswahili pia hutumika kiulizi kama ĉu, yaani je.)
Angalia kama viulizi vya
Kiesperanto hutumika mwazoni kabisa mwa maswali, bali viulizi vya Kiswahili
hutumika mwishoni:
Kion vi portis al mi?
|
Umeniletea
nini?
|
lakini,
pia:
|
|
Kiu
rompis ĉi tiun plumon?
|
Nani aliyeivunja kalamu hii?
|
Kiu plumo estas (la) via?
|
Kalamu
ipi ni yako?
|
ANGALIA
pia kwamba kwa Kiesperanto sentensi bila kiulizi chochote siyo kabisa swali:
La
bano estas preta.
|
Maji
ya kuoga ni tayari.
|
|
|
Ĉu la bano estas preta?
|
(Je,) Maji ya kuoga ni tayari?
|
Inawezekana kujibu:
|
|
Jes, ĝi estas preta.
|
Ndiyo,
tayari.
|
au
|
|
Ne,
ĝi ne estas preta.
|
Hapana.
Si tayari.
|
hii
ndiyo sababu ikawa si swali sentensi "La hundo kuras?",
kwa hivyo yafaa ujikumbushe kutumia kila mara kielezi Ĉu au
vielezi vyenye herufi K. mwanzoni ukiulizia swali!
37. ZOEZI
Ukiulizwa:
|
Ĉu li dancas?
|
Je, anacheza dansi?
|
unaweza kujibu:
|
Jes,
li dancas.
|
Ndiyo, anacheza dansi.
|
au:
|
Ne, li ne dancas.
|
Hapana,
hachezi dansi.
|
|
|
|
Pia
swali:
|
Ĉu
la birdoj kantas?
|
Je, wale ndege wanaimba?
|
linataka jibu:
|
Jes,
ili kantas.
|
Ndiyo, wanaimba.
|
au:
|
Ne, ili ne kantas.
|
Hapana,
hawaimbi.
|
Sasa
jibu wewe mwenyewe, halafu tafsiri maswali na jibu: Ĉu la nokto (usiku) estas
longa ? Ĉu la kuzoj (mtoto mwanamume wa ndugu wa mzazi mmoja; binamu) estas junaj?
38. MISEMO AKALI
Jifunze majibu haya yafuatayo:
Ĉu mi estas prava?
|
Nina haki? (au: Nimesema kweli? au: Nimesema vizuri?)
|
MAJIBU:
|
|
Jes. Kompreneble vi estas.
|
Ndiyo. Bila shaka.
|
Kompreneble ne.
|
Hasa siyo. Hakika siyo.
|
Eble
jes.
|
Pengine ndiyo. Huenda
ndiyo.
|
Eble
ne.
|
Labda siyo.
|
Efektive, vi estas
malprava.
|
Kwa kusema kweli umekosea.
|
39. MISEMO MINGINE
Jifunze majibu haya mengine:
Ĉu
li estas tie?
|
Yuko? Yupo? Yumo?
|
MAJIBU:
|
|
Eble
jes.
|
Labda
yuko.
|
Kompreneble ne.
|
Hasha,
hayuko.
|
Se jes, li...
|
Kama
yuko, a-......
|
Se ne, li ...
|
Kama
hayuko, a-.......
|
40. MASWALI
Jifunze
namna ifuatayo ya kuuliza:
Li
estas tie, ĉu ne?
|
Yupo au sivyo?
|
Li ne
estas tie, ĉu?
|
Hayupo au sivyo?
|
Yafaa ukumbuke kwamba neno ne likitumikwa katika
sentensi yenyewe, mara mengi neno hilo halitakiwi mwishoni.
41. ZOEZI
Tafsiri:
Kiu legas? La kuzo legas. –
Al kiu li legas? Li legas al mi. - Kia li estas. Li estas bona. -
Kie li estas? Li estas en la ĉambro. - Kio li estas? Li estas lernanto. -
Kio estas tio? Ĝi estas nur (tu) libro. - Kia
estas la libro? Ĝi
estas granda. - Kie ĝi estas ? Ĝi estas sur la tablo. - Ĉu la vojo (njia) estas
longa? Ne, ĝi ne estas longa: ĝi estas tre (sana) mallonga.
42. KIAMBISHITAMATI -IS
Umeshasoma
kwamba maneno yanayoonyesha tendo lile latendeka wakati huu wa sasa au kwa
kawaida yana kiambishi tamati -as. Ili kuonyesha wakati
uliopita wa kitenzi hutumika kiambishi -is:
mi estis
|
nilikuwa
|
mi ripozis
|
nilipumzika
|
mi laboris
|
nilifanya
kazi
|
mi venis
|
nilikuja
|
mi ludis
|
nilicheza
|
mi vokis
|
niliita
|
La infano ludis.
|
Yule
mtoto alicheza
|
La
viroj laboris.
|
Wale
wanaume walifanya kazi.
|
Li estis tie, ĉu ne?
|
Alikuwa pale, sivyo?
|
Ĉu li venis?
|
Je,
alikuja?
|
Ĉu vi ripozis?
|
Je,
ulipumzika?
|
43. ZOEZI
Rudia
sentensi za vifungu vya 27, 28 na
30 ukitumia alama ya wakati uliopita badala
ya kila alama ya wakati uliopo, halafu tafsiri sentensi hizo mpya.
Kwa mfano:
Mi
sidas kaj skribas. Ninakaa
na ninaandika.
Mi
sidis kaj skribis. Nilikaa na niliandika.
44. KIKATI -IN-
Kiambishi
hicho hutiwa katikati ya maneno yenyewe ili kuonyesha kwamba maneno hayo
yanahusu watu au wanyama wa kike, kwa hivyo kama patro ni "baba", "mama" ni patrino.
bovo
|
ng'ombe
dume
|
bovino
|
ng'ombe
jike
|
ĉevalo
|
farasi
dume
|
ĉevalino
|
farasi
jike
|
reĝo
|
ufalme
|
reĝino
|
malkia
|
45. ZOEZI
Tunga
sentensi kulingana na mfano huu:
avo kaj avino = babu kwa nyanya
ukitumia
maneno yafuatayo:
filo, frato, kato, knabo,
kuzo, lernanto, amiko, patro, onklo (ami, mjomba), ŝafo
(kondoo), viro, edzo.