4. SOMO LA NNE
24. KITENZI
Kitenzi kinaonyeshwa kwa kiambishi cha mwishoni -i kinachofanya kazi ile ile ya kiambishi awali cha Kiswahili ku-:
danci |
kucheza dansi |
legi |
kusoma |
dormi |
kulala (usingizi) |
ludi |
kucheza |
esti |
kuwa |
plori |
kulia (machozi) |
kanti |
kuimba |
ridi |
kucheka |
kuri |
kupiga mbio, kuimbia |
sidi |
kukaa, kuketi |
kuŝi |
kulala (chini) |
skribi |
kuandika |
labori |
kufanya kazi |
stari |
kusimama |
Lakini angalia kwamba unapotumia neno la kitenzi lenye kiambishi awali ku ili kuonyesha kitenzi kinapofanya kazi
ya jina peke yake, kwa Kiesperanto hutumika neno lenye kiambishi cha mwishoni -o:
Kuimba kwa Juma ni kubaya. |
La kanto de Ĝumo estas malbela. |
25. KIAMBISHI TAMATI -AS
Kiambishi kinachoonyesha kwamba tendo latendeka wakatí huu wa sasa, au kwa kawaida.
Nikisema La pano estas sur la tablo, ninafikiri wakati huu huu wa sasa. Angalia pia kwamba nikisema kwa Kiswahili
"nimelala" ninafikiri wakati huu wa sasa sawasawa na "ninalala" au "nalala"; kwa hiyo:
Li dormas = Analala, Alala, Hulala, Amelala
Li staras = Anasimama, Asimama, Husimama, Amesimama
26. MTENDAJI
Mifano ya kifungu cha 25 yakuonyesha kwamba kwa Kiesperanto haitumiki kiwakilishi cha
mtendaji kama a- (alala, analala, amelala = Li dormas) bali hutumika neno
la li, yaani lazima kutaja kila mara jina lenyewe la mtendaji au badala
yake maneno haya:
MI = mimi, ni-, n-, si-
VI = wewe, u-, w-, hu-
LI = yeye, a-, yu-, n.k. (kwa wanaume tu)
SI = yeye, a-, yu-, n.k. (kwa wanawake tu)
ĜI = yeye, ki-, i-, n.k. (kwa vitu na wanyama)
NI = sisi, tu-, tw-, hatu-
VI = ninyi, m-, mw-, ham-, hamw-
ILI = wao, wa-, vi-, zi-, n.k.
27. ZOEZI
Tafsiri kwa Kiswahili:
Mi sidas kaj skribas. Li kuŝas kaj ripozas (kupumzika). Ni staras kaj legas.
Ŝi estas en la ĉambro. Kie ĝi dormas? Mi sidas. La hundoj kuras.
La birdoj flugas (-ruka). La
kato kuŝas sur la lito. La knabo dormas en la lito.
28. ZOEZI
Kiu estas vi? Wewe ni nani?
Mi estas Aŝa. Mimi ni Asha.
Tafsiri kwa Kiswahili:
Kiu kantas? Ŝi kantas. - Kiu estas malbona knabo? Li. -
Kiu parolas (-ongea, -zungumza)?
Vi.
29. NENO NE
Neno hilo ndilo la kukanusha. Kwa Kiswahili habari ya kutotenda huonyeshwa kwa
mabadiliko ya maneno ya matendo: ninasoma - sisomi; anafanya kazi -
hafanyi kazi; kwa Kiesperanto lazima tutumie neno la kukanusha ne mara
moja kabla ya jina la matendo (au jina lolote la kukanushia). Angalia katika
sentensi zifuatazo jinsi neno la kukanusha linavyotumika:
Mwalimu hasimami. |
Instruisto ne staras. |
Walimu hawasimami. |
Instruistoj ne staras. |
Moyo ule haupigi. |
La koro ne batas. |
Mioyo ile haipigi. |
La koroj ne batas. |
Chakula hakitoshi. |
Manĝaĵajo ne sufiĉas. |
Vyakula havitoshi. |
Manĝaĵajoj ne sufiĉas. |
n.k. |
k.t.p. (kaj tiel plu) |
30. ZOEZI
Tafsiri kwa Kiswahili:
La pano ne sufiĉas. Ĝi ne estas freŝa. Ŝi ne estas bela,
sed ŝi ne estas malbela.
Ili ne ploras, ili ridas. Vi ne laboras,
vi ludas. Mi ne staras sur la benko,
ni sidas sur ĝi.
31. VlONGEZI
Kwa
Kiswahili maongezo ya maana ya sentensi inawezekana kupatikana kwa kubadili
mwisho wa kitenzi (hasa kwa jinsi ya kufanyia) au kwa kutumia maneno kama kwa, na, kwa ajili ya, kabla ya, baada ya,
karibu na, juu ya, chini ya, n.k. maneno haya yaitwa kwa Kiesperanto "prepozicioj" na katika sarufi hii
tutayaita "viongezi" kwa Kiswahili. Kiongezi ni namna moja ya
viunganishi.
32. APUD = karibu na
Tafsiri
kwa Kiswahili:
La teo estas apud la kafo. La hundo dorrnas apud la fenestro. Li sidas apud ŝi. La lito staras
apud la muro.
33. SUB = chini ya
Tafsiri kwa Kiswahili:
Ili sidas sub la luno. La planko estas sub la plafono.
La skatolo (mkebe) estas sub la tablo.
34. AL
Al huwa inaonyesha jinsi ya kufanyia tendo lenyewe lilivyo. Kwa kusema kweli
mara nyingi vitenzi vya kufanyia haiwezekani kuvitafsiri kwa kutumia kiongezi al.
Chungua sentensi zifuatazo:
Ninakutakia...
|
Mi
deziras al vi...
|
Tunawasomea.
|
Ni
legas al ili.
|
Unamzungumza nani?
|
Al
kiu
vi parolas?
|
Ninakwenda sokoni.
|
Mi
iras al bazaro.
|
Ametuletea machungwa.
|
Li
portis oranĝojn al ni.
|
LAKINI
Ametununulia machungwa.
|
Li aĉetis oranĝojn por ni.
|
Utuombee!
|
Preĝu
por ni!
|
Msinilililie mimi, bali jililieni nafsi zenu
na watoto wenu.
|
Ne
ploru pro mi, sed ploru pro vi mem kaj pro viaj infanoj.
|
Kumtolea Mungu sadaka.
|
Oferi
je Dio.
|
Ninakusalimia.
|
Mi
salutas vin.
|
35. ZOEZI
Tafsiri kwa Kiswahili:
Ili
kuras al ni. Ŝi kantas al li, sed li ne kantas al ŝi. La hundoj kuras
al la knabo. La birdoj flugas al la arbo.