3. SOMO LA TATU
12. KIAMBISHI AWALI MAL-
Kiambishi hiki
kinafanya kazi sawasawa ya irabu -u-
katika maneno yafuatayo toka Kiswahili:
kufunga
|
(fermi)
|
kufungua
|
(malfermi)
|
kuficha
|
(kaŝi)
|
kufichua
|
(malkaŝi)
|
yaani kiambishi hiki huyageuza maneno ili
kuonyesha kinyume cha maneno yenyewe. Angalia kwamba kiambishi hicho hutumika
kwa maneno ya aina yoyote kwa Kiesperanto:
juna
|
-changa
|
maljuna
|
-zee, -a kizee
|
luma
|
-enye nuru, -angavu
|
malluma
|
-a giza, -eusi
|
ordo
|
utaratibu
|
malordo
|
fujo
|
amo
|
mapenzi
|
malamo
|
chuki
|
Basi, kinyume
cha maneno mengine uliyojifunza mpaka sasa ni:
maldika
|
-embamba
|
malgranda
|
-dogo
|
mallonga
|
-fupi (kwa kwenda mbele)
|
malplena
|
-tupu
|
malsana
|
-gonjwa
|
|
|
na kadhalika...
mola
pano
|
mkate mororo
|
malmola
pano
|
mkate mkavu
|
pura
akvo
|
maji safi
|
malpura
akvo
|
maji machafu
|
bona
knabo
|
mvulana mwema
|
malbona
knabo
|
mvulana mbaya
|
13. ZOEZI
Soma ukatafsiri kwa Kiswahili:
Malalta
plafono. Malbela viro. Malbona banano (ndizi).
Maldika glaso. Malforta fadeno. Malgranda
filo. Mallonga krajono. Malnova kajero (daftari). Malplena glaso. Malpura objekto. Malsana frato. Malvarma loko. Malbela
libro. Maljuna hundo (mbwa). Malkontenta
kato (paka).
14. KIAMBISHI -J
Kiambishi hiki ni kiwakilishi cha wingi.
Kwa
Kiswahili mabadiliko ya jumla yahitaji mabadiliko ya ngeli ya jina: mtu mmoja (jumla ya umoja), watu
wengi (jumla ya wengi/wingi).
boto
|
buti (kiatu kirefu)
|
botoj
|
maboti
|
lando
|
nchi
|
landoj
|
nchi
|
mano
|
mkono
|
manoj
|
mikono
|
patro
|
baba
|
patroj
|
mababa
|
tempo
|
wakati
|
tempoj
|
nyakati
|
viro
|
mwanamume
|
viroj
|
wanaume
|
15. ZOEZI
Rudia maneno ya vifungu vya 6 na 10 katika
wingi kama mfano ufuatao:
(Amiko)
Amikoj. Marafiki.
16. MIUNGANO -AJ -OJ
Kiambishi cha wingi j hutumika pia
mwishoni pa vivumishi katika vikundi kama hivi:
la
ruĝaj libroj
|
vile vitabu vyekundu
|
basi katika umoja tunavyo viambishi -a
-o lakini katika wingi tunayo miungano ya viambishi -aj -oj.
17. UPANGAJI WA VIVUMISHI
Kwa utokezo wa mazoeza vivumishi hutangulia
jina zinalolisifu:
vile vitabu vipya vyekundu kumi
la
|
dek
|
novaj
|
ruĝaj
|
libroj
|
|
kumi
|
vipya
|
vyekundu
|
vitabu
|
lakini hakuna sheria hasa juu ya upangaji wa
sifa hizi za mchanganyiko katika sentensi.
18. ZOEZI
Rudia vifungu vya 9 na 13 katika wingi kama
mfano ufuatao:
Altaj tabloj
|
Meza ndefu
|
La malbelaj viroj
|
Wale wanaume wasio wazuri
|
19. KUMBUKA!
Wingi wa vitu (au jina lolote) huonyeshwa kwa
kuweka kiambishi j mwishoni pa jina na pa kivumishi cha sifa (kikiwapo),
lakini siyo mwishoni pa "kibainihakika" la.
20. NENO ESTAS
Estas maana yake
ni (na "yu, u, m, wa,"
n.k.):
La
tasko estas simpla.
|
Kazi ile ni rahisi.
|
La
taskoj estas simplaj.
|
Kazi zile ni rahisi.
|
La
vortoj estas longaj.
|
Maneno yale ni marefu.
|
La
forkoj estas akraj.
|
Nyuma zile ni/zi kali.
|
La
plankoj estas lignaj.
|
Sakafu zile ni/zi za miti.
|
La
benkoj estas malnovaj.
|
Viti vile ni/zi vigumu.
|
ANGALIA! Mara nyingi kwa Kiswahili haitakiwi
kitenzi kuwa (yaani maneno ya ni, yu, ki, u, m, n.k.): ukisema
"Juma mfalme", "Asha mwanamke'', neno lile "ni" au
"yu", n.k., linafichika (yaani limo katika fikira zako tu).
Kwa Kiesperanto lazima utie kila mara neno hilo
kati ya maneno mawili haya ya sentensi zilizoonyeshwa, yaani:
Ĝumo
estas reĝo.
|
Juma mfalme.
|
Aŝa
estas virino.
|
Asha mwanamke.
|
21. JIFUNZE MANENO HAYA:
kaj= na
sed = lakini, bali
ne estas = si
de = -a(yaani: cha, vya, mwa, wa, ya, n.k.)
en = katika, ndani ya, -ni:
-ni:
|
Estas kafo en la taso.
|
Mna kahawa kikombeni mle.
|
sur = juu ya, -ni:
-ni:
|
La libro de Ĉilongo estas sur la tablo.
|
Kitabu cha Chilongo kipo mezani pale.
|
22. ZOEZI
Tafsiri kwa Kiswahili ukilingana na mfano:
Mfano: La nomo de la viro estas Ernesto.
Jina la yule mwanamume ni Ernesto.
La floro estas freŝa (-bichi).
La pano ne estas freŝa (-pya,
-tefu). La ŝafo (kondoo) ne estas granda. La ŝafoj ne estas
grandaj. En la libro estas bildo (picha). En la libro estas bildoj. La libro de la knabo estas sur la planko. La
fiŝo (samaki) estas en la akvo.
La viroj estas en la ŝipo (meli). La
libro kaj la pIumo estas sur la tablo. La patro estas bona, sed la frato estas
malbona.
23. ZOEZI
Jibu maswali haya kwa kutumia sentensi za
kifungu cha 22. Baadaye tafsiri.
Kio estas sur la tablo? Kio
estas en la libro? Kio estas sur la planko? Kio estas en la
ŝipo ?
Kie
= wapi?
|
Tie
= pale, kule, mle.
|
Kie estas la libro de la knabo? La libro de la knabo
estas tie sur la planko.
Kie
estas la fiŝo? Kie estas bildoj? Kie estas la libro kaj la plumo? Kie estas
la viroj?
Kie
estas la floro? Kie estas la ŝafo? Kia estas la
pano? Kia estas la patro?
Je, ulitumia pia kiambishi awali mal
katika majibu yako
|