YALIYOMO * Utangulizi
Notice: Undefined variable: function_ret in /var/www/vhosts/vessella.it/httpdocs/fpdb/esp/yaliyomo.inc.php on line 18
* Somo la kwanza
Notice: Undefined variable: function_ret in /var/www/vhosts/vessella.it/httpdocs/fpdb/esp/yaliyomo.inc.php on line 18
* Somo la pili
Notice: Undefined variable: function_ret in /var/www/vhosts/vessella.it/httpdocs/fpdb/esp/yaliyomo.inc.php on line 18
* Somo la tatu
Notice: Undefined variable: function_ret in /var/www/vhosts/vessella.it/httpdocs/fpdb/esp/yaliyomo.inc.php on line 18
* Somo la nne
Notice: Undefined variable: function_ret in /var/www/vhosts/vessella.it/httpdocs/fpdb/esp/yaliyomo.inc.php on line 18
* Somo la tano
Notice: Undefined variable: function_ret in /var/www/vhosts/vessella.it/httpdocs/fpdb/esp/yaliyomo.inc.php on line 18
* Somo la sita
Notice: Undefined variable: function_ret in /var/www/vhosts/vessella.it/httpdocs/fpdb/esp/yaliyomo.inc.php on line 18
* Somo la saba
Notice: Undefined variable: function_ret in /var/www/vhosts/vessella.it/httpdocs/fpdb/esp/yaliyomo.inc.php on line 18
* Somo la nane
Notice: Undefined variable: function_ret in /var/www/vhosts/vessella.it/httpdocs/fpdb/esp/yaliyomo.inc.php on line 18
* Somo la tisa
Notice: Undefined variable: function_ret in /var/www/vhosts/vessella.it/httpdocs/fpdb/esp/yaliyomo.inc.php on line 18
* Somo la kumi
Notice: Undefined variable: function_ret in /var/www/vhosts/vessella.it/httpdocs/fpdb/esp/yaliyomo.inc.php on line 18
* Kamusi
Notice: Undefined variable: function_ret in /var/www/vhosts/vessella.it/httpdocs/fpdb/esp/yaliyomo.inc.php on line 18
Notice: Undefined variable: function_ret in /var/www/vhosts/vessella.it/httpdocs/fpdb/esp/yaliyomo.inc.php on line 43
|
2. SOMO LA PILI
4. KIBAINIHAKIKA
Kibainihakika
ni neno linaloleta dhana ya uhakika. Kwa Kiesperanto hutumika neno la
ambalo huja kwanza katika fungu la maneno (yaani fungu la majina linayoyaletea
"uhakika"). Matumizi ya neno hili yanaonyesha kitu (au vitu) fulani
kilichokwisha tambulishwa, au kinachojulikana:
Daresalamo estas urbo.
|
Dar es Salaam ni mji (kama Nairobi, Kinshasa, Maputo, ... n.k.)
|
|
|
La urbo estas bela.
|
Mji
ule (uliotajwa, yaani: Dar es Salaam, siyo mji mwingine) ni mzuri.
|
Kwa Kiswahili inawezekana kubainisha uhakika wa kitu fulani kwa njia ya
vionyeshi au viashirio (yaani: ule, yule,
kile,... n.k.), lakini ni muhimu kutambua wazi kwamba dhana ya
"uhakika" katika Kiswahili ni tofauti kidogo na dhana ya
"uhakika" katika Kiesperanto.
Ni dhahiri kwamba ikiwa tunataja jina la pekee (kama Juma, Nairobi, Luanda, Esperanto, Afrika,
Kitaru, Abdallah, n.k.) hatutumii kibainihakika, kwa sababu jina la namna
hiyo lina dhana ya uhakika ndani mwake mwenyewe.
5. MUUNDO WA MANENO
Kila neno la Kiesperanto lina sehemu (au mofimu) mbali mbali. Sehemu kuu
yaitwa mzizi. Huu mzizi ndio kiini cha neno kwa jumla, yaani unaonyesha maana
ya asili ya neno lenyewe. Sehemu ya pili ni mwisho wa neno (iitwayo kiambishi
tamati) unaoonyesha kazi za neno lenyewe katika sentensi na aina yake. Sehemu
nyingine ni kiambishi awali na viambishi vya ndani (viitwavyo vikati pia):
neno:
|
jes (ndiyo)
|
lina
|
mzizi:
jes tu,kiambishi-tamati
kimefichwa (tunasema kwamba ni cha kisifuri)
|
|
bela (-zuri)
|
|
mzizi
(yaani: bel) na kiambishi tamati
(yaani: a)
|
neno:
|
malbela (-baya)
|
lina:
|
mzizi
(bel), kiambishi tamati (a) na kiambishi awali (mal)
|
|
malbeleta (-baya kidogo)
|
|
mzizi: bel
kiambishi awali: mal
kiambishi cha ndani: etkiambishi tamati: a
|
|
malbelulino (mwanamke asiye mzuri)
|
|
mzizi:
bel
kiambishi awali: mal
kiambishi
cha ndani: ul
kiambishi
cha ndani: in
kiambishi
tamati: o
|
Matumizi
ya viambishi hivi yanaleta mabadiliko ya maana, ya aina ya neno, na ya kazi ya
neno katika sentensi. Mabadiliko yo yote yahitaji kila mara mabadiliko ya
kiambishi:
mtoto
|
watoto
|
kitoto
|
utoto
|
kijitoto
|
infano
|
infanoj
|
infane
|
infaneco
|
infaneto
|
mtu
|
watu
|
utu
|
jitu
|
kimtu
|
homo
|
homoj
|
homeco
|
homego
|
home
|
6. KIAMBISHI -O
Kiambishi
hiki cha mwisho hutumika kuonyesha jina (la kitu au la mtu, la mahali au la
jambo, la matendo au la hali, au la kiumbe cho chote):
amiko
|
rafiki
|
frukto
|
tunda
|
muro
|
ukuta
|
arbo
|
mti
|
homo
|
mtu
|
oranĝo
|
chungwa
|
besto
|
mnyama
|
kafo
|
kahawa
|
patro
|
baba
|
bildo
|
picha
|
konsilo
|
shauri
|
pordo
|
mlango
|
ĉambro
|
chumba
|
libro
|
kitabu
|
rozo
|
waridi
|
edzo
|
mume
|
lito
|
kitanda
|
tablo
|
meza
|
fadeno
|
uzi
|
loko
|
mahali
|
tago
|
siku
|
filo
|
mwana
|
luno
|
mwezi
|
teo
|
chai
|
floro
|
ua
(maua)
|
meblo
|
fenicha
|
viro
|
mwanamume
|
7. ZOEZI
Soma
ukatafsiri kwa Kiswahili:
Kio estas tio? (Hiki ni nini? Hiki ni kitu gani?) Tio estas pordo. Kio estas kato (paka)?
Kato estas besto. Kio estas tablo?
Tablo estas meblo. Kio estas oranĝo? Oranĝo estas frukto. Kio
estas rozo?Rozo estas floro.
(Jina unalotumia kwa kujibu neno kio lazima liwe na kiambishi tamati o).
8. KIAMBISHI -A
Kiambishi tamati hiki hutumika kuonyesha neno linalosifu jina au
huonyesha namna ya mtu au ya kitu fulani. Neno lenye kiambishi tamati hicho
huitwa "kivumishi cha sifa" au kivumishi tu. Kwa Kiswahili maneno
mengi yaliyoonyesha namna ya jina hayapatanishi ngeli ya jina yanalolisifu,
bali kwa Kiesperanto kila neno linaweza kufanya kazi ya kivumishi kwa
kubadilika tu kiambishi tamati.
mtu mrefu (urefu wa kwenda juu)
|
alta homo
|
mtu
wa saburi
|
pacienca homo
|
mtu
mwenye mali, tajiri
|
riĉa homo
|
Angalia mafungu yafuatayo
yule
mtu ni mrefu
|
la homo estas alta
|
bilauri
iliyojaa
|
plena glaso
|
ile
bilauri iliyojaa
|
la plena glaso
|
ile
bilauri imejaa
|
la glaso estas plena
|
darasa
kubwa
|
granda klaso
|
lile
darasa kubwa
|
la granda klaso
|
lile
darasa ni kubwa
|
la klaso estas granda
|
Ujifunze vivumishi vya hapa chini
bela
|
-zuri
|
bona
|
-ema
|
dika
|
-nene
|
forta
|
-enye
nguvu, kali, imara
|
granda
|
-kubwa
|
kontenta
|
-radhi,
-furahifu
|
longa
|
-refu
(urefu wa kwenda mbele, au wa muda)
|
mola
|
-ororo,
-tefu
|
nova
|
-pya
|
pura
|
safi
|
sana
|
-zima,
-enye afya
|
varma
|
-enye
joto, -a moto
|
vera
|
-a kweli
|
verda
|
-enye
rangi ya kijani
|
9. ZOEZI
Andika
sentensi kwa kutumia maneno la na
estas kama mfano ufuatao:
Alta tablo (meza ndefu)
|
La alta tablo.
|
|
La tablo estas alta!
|
Sasa tafsiri sentensi ulizoziandika.
Bela floro. Bona konsilo.
Dika muro. Forta viro. Granda bildo. Kara (mpendwa) patro. Longa tago. Mola lito. Nova luno.
Pura loko. Sana homo. Verda libro. Longa fadeno. Vera amiko. Alta arbo.
10. MANENO AKALI
Angalia matamko ya miungano ya herufi katika maneno haya:
frato
|
kaka,
ndugu
|
fenestro
|
dirisha
|
glaso
|
bilauri,
gilasi
|
klaso
|
darasa
|
pupitro
|
meza,
deski
|
lernanto
|
mwanafunzi
|
instruisto
|
mwalimu
|
kreto
|
chaki
|
frukto
|
tunda
|
stelo
|
nyota
|
bildo
|
picha
|
birdo
|
ndege
|
krajono
|
kalamu,
pensili
|
pIumo
|
unyoya,
kalamu ya wino
|
plafono
|
dari,
sakafu ya juu
|
objekto
|
kitu
|
11. ZOEZI
Kia estas la fadeno? Ule uzi ni wa namna gani?
La fadeno estas longa.
Ule
uzi ni mrefu.
Jibu
maswali yafuatayo kwa kutumia neno lenye kiambishi tamati a:
Kia estas la pordo? Kia estas la plafono? Kia estas la pIumo?
Kia estas la bildo? Kia estas la tago? Kia estas la
krajono?Kia estas la kafo? Kia estas la lito? Kia estas la
floro? Kia estas la teo?
|